NIMUHIMU KUJIFUNZA TAKWIMU NA SENSA ZA WATU

Na Mahmoud Ahmad Arusha

WANAFUNZI wa skulli za sekondari nchini wamehimizwa umuhimu wa kujifunza takwimu na sensa ya watu na makazi ili kuelewa umuhimu wake katika mipango na vipaumbele vya taifa katika kutoa huduma kwa wananchi wake.

Mratibu wa Sensa ,mkoa wa Arusha, Dk. Magreth Martin, ameyasema hayo ,alipokuwa akitoa elimu ya sensa na takwimu kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa skuli ya sekondari ya Longido,waliokuwa wakipata elimu ya sensa ya watu na makazi mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.

Dk, Martin, amewaambia wanafunzi hao kuwa ofisi ya Sensa na Takwimu, inawezesha taifa kufahamu idadi ya watu wake,mahitaji  na hivyo kuandaa  mipango kulingana na mahitaji  ya watu na pia takwimu zinawezesha  taifa kuwa na mipango  ya maendeleo  na kuelewa hali halisi ya uchumi na mfumko wa bei ya bidhaa.

Amewaambia kuwa wakati wa sense ya kuhesabu watu taifa hugawanywa kwenye maeneo madogo madogo ili kurahisisha zoezi hilo na hivyo kupata idadi kamili ya watu na kufahamu mahitaji halisi ya eneo husika .

Dk. Martini,amesema wakati wa zoezi hilo la sensa huwa wanakumbana na changamoto mbalimbali kutegemeana na mazingira ,itikadi ya kisiasa na dini ambapo baadhi ya watu huwa hawataki kuhesabiwa kutokana na dhana potofu kuwa kuhesabiwa ni kuchuliwa mabaya jambo ambalo halihusiani kabisa.

Amewaambia kuwa kabla ya kuanza zoezi hilo hufanyika zoezi la majaribio ambalo hufuatiwa na upatikanaji wa vifaa ,ikiwemo madodoso ,kutengwa kwa maeneo ya kuhesabia na kuandaliwa maswali yanayoeleweka .

Amesema Kaya zenye familia kubwa ndizo zinaongoza kwa umaskini kutokana na kutokuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi kuhudumia familia nziwa wakati Kaya yenye familia ndogo ya watu inakuwa na maisha bora na huduma inapatikana .

Amesema kulingana na utafiti umaskini wa watanzania unazidi kuongezeka  kutokana na kaya kuwa na idadi kubwa ya watu ambao hawapati huduma muhimu na za lazima kwenye familia kubwa inakabiliwa na umaskini, wa kipato,kielimu, upungufu wa mlo na huo ndio chimbuko la umaskini

Ametoa wito kwa shule zingine kushirikiana na ofisi hiyo ya Sensa ili kuwezesha kuwajengea uwezo wanafunzi kuelewa umuhimu wasensa ya watu na makazi yao na hivyo kupata takwimu zitakazosaidia  kupunguza umaskini kwenye kaya.

Mwakilishi wa wanafunzi hao, Magerthi Chagula, amesema  mara baada ya mafunzo hayo yasiku mojaambayo yamewajengea uelewa mkubwa wataenda kuwa mabalozi kwenye maeneo wanakotoka ili kuelimisha jamii kuzingatia umuhimu wa uzazi .

Amesema wingi wa watoto kwenye familia ni mzigo na hivyo kuongeza umaskini  ambalo ni tatizo kubwa na kuacvha kutumiawatoto kama nguvu kazi badala yake watoto waruhusiwe kwenda shule.

Kwa upande wake kiongozi wa jopo la walimu wa shule hiyo, Mwalimu Eunice Ikonje, amesema mafunzo hayo yatawasaidia kujifunza zaidi yawalivyotarajia .

Amesema mafunzo hayo yamewajengea uyelewa na mwamko mkubwa wa kuelewa umuhimu  wasensa na takwimu kwa ajilli ya maendeleo  ya taifa .

Aidhaameiomba ofisi hiyo yasensa kutembelea shule mbalimbali ili kutoa elimu hiyo ya sense na takwimu ili kuwajengea uelewa wanafunzi

Dakta Martini, amekuwaakitoaelimu yasensa na takwimu kwa shule mbalimbali ambapo tayari shule zaidi ya kumi zimeshanufaika na elimu hiyo.

0 Comments