PROF NDALICHAKO ACHANGIA SH 4.5 MILIONI TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

Kwa ufupi

Misaada iliyokabidhiwa leo asubuhi ni pamoja na kanga, sabuni za kuogea na kufulia, dawa za meno, juisi, maji ya kunywa, pampers na mabeseni.

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefanya usafi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 4.5 milioni katika Taasisi ya Satarani ya Ocean Road.

Misaada iliyokabidhiwa leo asubuhi ni pamoja na kanga, sabuni za kuogea na kufulia, dawa za meno, juisi, maji ya kunywa, pampers na mabeseni.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Profesa Ndalichako alisema katika kusherehekea wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) waliadhimia kuwatembelea wanawake wanaotibiwa saratani.

“Tunatambua kwamba wana mahitaji pia, kama ilivyo wanawake ndiyo nguzo ya maendeleo kwa hiyo anavyougua kwa muda mfupi familia hutetereka, tumekuja hapa na vifaa mbalimbali ambavyo tunaamini hawa wagonjwa wanavihitaji,” amesema Profesa Ndalichako

2

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na viongozi wa hospitali hiyo muda mfupi baada ya kuwasili katika hospitali hiyo.

34

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlojia Profesa Joyce Ndalichako akiwajulia hali wagonjwa mbalimbali ambao alifika kuwajulia hali pamoja na kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

0 Comments