Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara Joel Chidabwa kawataka wanawake wa Mkoa wa Mtwara kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Amesema hayo mapema mkoani Mtwara alipokuwa akifungua mafunzo hayo kwa wanawake wajasiriamali katika sekta ya vipodozi na urembo. Mafunzo hayo yanatolewa bure kwa wanawake 30 waliotuma maombi na kuchaguliwa na Taasisi ya Manjano Foundation.
Akieleza zaidi amesema “Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake kupata elimu ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia bidhaa hizo”
Baada ya kuhitimu mafunzo haya washiriki hao wataunganishwa na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ya kupata mitaji ya kuanzisha bishara.
Mwezeshaji Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation Bi Ester Lukindo Akizungumza Machache wakati wa Uzinduzi Huo.
Bi Ester Lukindo aliyesoma hotuba kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama “Shekha Nasser alisema kuwa "wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo."
Washiri wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi.
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi Mtwara ukiwa ni mkoa wa tatu tayari kufikiwa.
0 Comments