Wanafunzi 20 wafariki katika ajali iliotokea mjini Pretoria nchini Afrika Kusini
Wanafunzi wenye umri kati ya miaka mitano na 10 wameripotiwa kufarika katika ajali iliotokea kaskazini mwa jiji ka Pretoria nchini Afrika Kusini Ijumaa.
Ajali hiyo imefahamishwa kutokea baada ya lori moja kupoteza muelekeo na kugonga basi lililokuwa na wanafunzi kaskazini mwa Pretoria.
Basi hilo la wanafunzi lilishika moto wakati wa tukio hilo.
Waziri wa uchukuzi wa Afrika Kusini Joe Maswanganyi ametuma salamu za rambirambi kwa wazazi wa watoto waliofariki katika ajali hiyo.
0 Comments