WANAFUNZI WA VETA WATEMBELEA MGODI WA DHAHABU - BULYANHULU


Wanafunzi wanaosoma katika Chuo Cha Ufundi – VETA Moshi mkoani Kilimanjaro wanasomea kozi maalumu kuhusu ufundi wa mgodini na viwandani wametembelea banda la mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kwenye maonesho ya wiki ya usalama na afya mahali pa kazi mwaka 2017.

Wakiwa katika banda hilo wamejionea namna mgodi huo unavyozingatia masuala ya afya na usalama kwa wafanyakazi mgodini ili kujiepusha na magonjwa na ajali zinazoweza kutokea wakiwa kazini.

Wanafunzi hao wanatoka katika vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Banda la Mgodi wa Bulyanhulu mwaka huu limetia for a kwa kutembelewa na wananchi,walimu,watalii kutoka nje ya nchi na wafanyakazi mbalimbali ambapo tangu Aprili 26,2017 mpaka leo Aprili 29,2017 zaidi ya watu 1200 wametembelea banda hilo.

Katikati ni Afisa Mahusiano Mgodi wa Bulyanhulu Mary Lupamba akielezea masuala ya afya na usalama mgodini kwa wanafunzi wanaosomeshwa na mgodi huo katika chuo cha VETA Moshi

Afisa Mahusiano Mgodi wa Bulyanhulu Mary Lupamba akisisitiza jambo kwa wanafunzi wanaosoma chuo cha Veta Moshi waliotembelea banda la mgodi huo

Wa pili kulia ni Afisa Rasilimali Watu Mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha akiwakaribisha walimu kutoka chuo cha VETA Moshi walioambatana na wanafunzi wao.Wa kwanza kushoto ni Mwalimu Esrom Lema akifuatiwa na mwalimu Emmanuel Kweka aliyevaa fulana zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu kwa ajili ya walimu wanaofundisha katika chuo hicho

Kushoto ni Afisa Mazingira Mgodi wa Bulyanhulu Digna Isdory na Afisa Rasilimali Watu Mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha wakizungumza na wanafunzi wa chuo cha VETA waliotembelea banda la mgodi huo

Afisa Rasilimali Watu Mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha akijiandaa kugawa fulana kwa wanafunzi 9 wanaosomeshwa na mgodi wa Bulyanhulu katika chuo cha VETA.

Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Mazingira Mgodi wa Bulyanhulu Digna Isdory akiendelea na zoezi la kugawa fulana kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha VETA Moshi waliotembelea banda la mgodi huo

Wanafunzi wanaosoma katika chuo cha VETA Moshi waliotembelea banda la mgodi wa Bulyanhulu wakivaa fulana walizopewa na mgodi huo

Wanafunzi wa chuo cha VETA wakivaa fulana zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu

Maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi 9 wanaosomeshwa na mgodi huo katika chuo cha VETA

Picha ya pamoja wanafunzi na maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu

0 Comments