SIMANZI KUBWA ARUSHA

Jiji la Arusha leo umepoa, kwasababu ya simanzi, majonzi na uchungu usiomithilika. Ni kwasababu ya vifo vya wanafunzi, walimu na dereva iliyotokea Rotia, Karatu.

Ndoto, vipaji na ubunifu wa wanafunzi hao ulikuwa unahitajika sana kwa taifa sasa na hapo baadae, tutakutana uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kuaga miili yao kisha kwenda kuwazika.

Hatuna cha kuongeza bali kutoa pole za dhati kwa watanzania wote, Mungu awalaze pema peponi.

0 Comments