WANAFUNZI TAKRIBANI 32 WANAHOFIWA KUFA KWENYE AJALI - ARUSHA



Kwa mujibu wa Hospitali ya Lutheran Karatu wanasema wamepokea maiti ya 32 ambao ni wanafunzi 29, walimu 2 na dereva 1 katika ajali ya basi la shule ya Luck Vicent ya Arusha Mjini iliyokuwa ikielekea Karatu kwaajili ya mitihani yakirafiki.

Habari zinaeleza kuwa  basi hilo limeanguka kabla ya kuingia karatu mjini na kuua watoto wengi .Inaarifiwa kuwa Wanafunzi hao  ni wa shule inayoitwa Lucky Vicent ya Arusha ambao walikua wanaenda karatu kufanya mitihani ya mashindano na shule za karatu.

0 Comments