Mwalimu Bora ni vitendo, huwapenda, huwajali, huwashauri, uwalea, huwafuatilia, hushirikiana na wanafunzi kimaisha kwa maendeleo na faida ya Taifa.
Nimejifunza katika ualimu wangu, kuta na mipaka ya shule havitenganishi mema, mazuri unayowekeza katika #Roho za wanafunzi wako.
Vijana hawa ni baadhi tumeshauriana tangu wakiwa secondari na sasa wapo Chuo Kikuu, tukishirikiana uzoefu wa kimaisha, kielimu, kijamii na kiuchumi.
Kuna kasumba iliyojengeka katika jamii kuwa mwalimu na mwanafunzi ili mambo yaende lazima uwe mkali, uchape sana, muwe maadui ili wanafunzi wafaulu, wakuheshimu na baada ya kuhitimu shule kila mtu na lake.
Nadhani ni wakati sasa walimu tubadilike na tujifunze kuwalea wanafunzi kwa kufuatilia, kuthamini na kuwajenga uwezo wa uelewa wa maisha toka Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu.
"Walimu wajitafakari namna yetu ya kujitoa kuwaonyesha njia Bora Wanafunzi wetu"
Tufuatilie kupitia, Instagram: @elimuafrika, Facebook: Elimu Afrika, Twitter: @ElimuAfrika na YouTube: Elimu Afrika.
#SiasaIsiingilieTaaluma.
0 Comments