Elimu Afrika imepokea kwa thamani ya juu mwaliko kwenye semina ya wakufunzi wa walimu wa watu wenye ulemavu (Viziwi), semina hii inahusu Walimu wa Shule za Msingi Wilaya ya Longido, wamekuja Shule ya Msingi Meru kitengo cha Elimu Maalum kujifunza Lugha ya Alama ili wakafundishe walimu wenzao waliobaki kwenye shule walizotokea.
Hili limekuja baada ya kugundulika wanafunzi wengi viziwi kufichwa na wazazi wao na kupelekea wao kukosa Elimu katika umri stahiki, kwa mfano; Kwa Wilaya ya Longido tu wamepatikana zaidi ya Viziwi 70 ambao wamekosa Elimu, hasa ya Lugha ya Alama ambayo ndio nguzo ya kuwapatia Elimu.
Hivyo taasisi ya ABILIS Foundation, Finnish Special Education in Africa na CHAVITA ambazo ndio wafadhili wa mafunzo haya ya walimu wakufunzi, ikaona ni vema kuwapa mafunzo walimu ili wakafundishe Lugha ya Alama walimu na wanafunzi kwenye shule wanazotoka, hili litasababisha watoto na watu wenye ulemavu wa kuto sikia (Viziwi) kutonyanyapaliwa na kuheshiwa na mfumo wa Elimu ya Tanzania.
Tunawapongeza sana idara ya Elimu Mkoa (ambao ndio walifungua mafunzo haya) kwa kulipokea na kukubali mafunzo haya kufanyika, shule ya msingi Meru, taasisi ya ABILIS Foundation, Finnish Special Education in Africa na CHAVITA kwa kuwapa fursa ya semina kwa walimu toka Wilaya ya Longido, nasi Elimu Afrika tumenufaika na semina hii sana kwa kujifunza Lugha ya Alama, maisha ya Viziwi, jinsi ya kufundisha kiziwi na mengine mengi.
Semina inaendelea hivyo endelea kutufuatilia kujua kitakachojiri.
"Jitahidi kujielimisha kwa kadri ya uwezo wako na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote"
Tufuatilie kupitia, Instagram, Facebook, Twitter,YouTube,
#SiasaIsiingilieTaaluma.
0 Comments