Kwa katuni;
Lazima Serikali iwe wazi kuwa "Elimu inayogharamiwa na Serikali" maarufu kwa jina la Elimu Bure imekuwa mzigo mkubwa kwa Serikali ni vema wazazi na wadau wakarejea mfumo wa zamani wa uchangiaji wa gharama za Elimu.
Imefikia mahali walimu wanafanyakazi bora liende, wazazi wamesusa maendeleo yakimasomo ya watoto wao, wadau wanahofu ya kuchangia elimu, serikali inadanganywa na takwimu za taasisi zinazotoa matokeo ya tafiti butu, vibali vya uchangiaji kuwa kisiasa zaidi.
Nipendekeze mfumo wa kuchangia gharama za Elimu ziendelee kama ilivyokuwa awali ili wadau wote wafuatilie kwa karibu thamani ya fedha yao kwenye matokeo yakimasomo kwa watoto wetu ambao ni taifa lijalo.
Wasomi Mungu anawaona! Wengi wanashindwa kusema ukweli ili wasipoteze fursa zao, Jamani eeh #ElimuyaTanzania ni #Janga tunahitaji kujirudi na kuipa umuhimu unaostahili tuache #blabla.
#Tafitizaelimuziwezakweli
Elimu Afrika
"Jitahidi kujielimisha kwa kadri ya uwezo wako na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote"
Tufuatilie kupitia, Instagram: @elimuafrika, Facebook: Elimu Afrika, Twitter: @ElimuAfrika na YouTube: Elimu Afrika na www.elimuafrikatz.blogspot.com #SiasaIsiingilieTaaluma.
0 Comments