WAKALA wa Taifa wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) umejipanga kutoa mafunzo na kuhamasisha wananchi kutumia teknolojia ya fremu mpya za milango zinazotengenezwa kwa kutumia zege.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Meneja wa Utafiti na Maendeleo NHBRA wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utafiti wa fremu za milango ya zege uliofanywa na wakala huo kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali ya ART Energy.
Alisema utafiti wa utengenezwaji wa fremu hizo ulianza Aprili mwaka huu na unaendelea hadi sasa na ulifanyika baada ya kubaini changamoto ya fremu za mbao katika nyumba nyingi.
Aliongeza kuwa utafiti huo ulibaini faida nyingi za uwepo wa milango hiyo katika nyumba ikiwemo kusaidia kupunguza matumizi ya miti kwa ajili ya kutengeneza fremu pamoja, kupunguza gharama za kununua fremu na kuepuka kuharibika haraka kwa fremu hizo ukilinganisha na fremu za mbao.
Pia alisema faida nyingine ni fremu hizo haziwezi kuathiriwa na unyevu wa maji yatokanayo na mvua, haziliwi na mchwa na ni rahisi kusafirishwa. Aidha alisema utengenezwaji wa fremu hizo hautofanywa na wakala huo pekee, bali watatoa ujuzi huo kwa watu wengine watakaopenda ili waweze kutengeneza na kuuza wao
0 Comments