TCU YATANGAZA SIFA MPYA ZA KUJIUNGA VYUO VIKUU

Kaimu Katibu Mtendaji TCU, Profesa Eleuther Mwageni 

Kwa ufupi

Akizungumza leo Julai 20, Kaimu Katibu Mtendaji TCU, Profesa Eleuther Mwageni amesema hawatapokea maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kama ilivyokuwa hapo mwanzo.

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema maombi ya kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yatatumwa moja kwa moja vyuoni.

Akizungumza leo Julai 20, Kaimu Katibu Mtendaji TCU, Profesa Eleuther Mwageni amesema hawatapokea maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kama ilivyokuwa hapo mwanzo. 

Maombi ya kujiunga na elimu ya juu yataanza kupokelewa rasmi Julai 22 kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu nchini.

"Wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu wasisite kuchagua vyuo wanavyovipenda na kuhakikisha wanakuwa makini na programu zilizowekwa na vyuo iwapo zinatambuliwa na Tume," Amesema.

Amesema TCU haitatoza ada yoyote ya udahili kwa waombaji.

0 Comments