WATOTO WASISITIZWE UBUNIFU

Ninaunga mkono ubunifu wa mpira wa makaratasi, ya soksi na ringi, zamani tulikuwa na utaratibu wa kubuni vitu kutengeneza vigari vya makopo na waya, mbao, matairi n.k

Nia ya kukumbusha hili si ili kupinga biashara ya vitu vya watoto vya plastiki maarufu kama vya kichina.

Nawaomba turejee kwenye kuwasisitiza watoto wetu kubuni vifaa vyao vya kuchezea kwasababu inawaandaa kujifunza na kutumia mazingira yao kwa manufaa ya sasa na ya baadae.

"Jitahidi kujielimisha kwa kadri ya uwezo wako na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote"

Tufuatilie kupitia Elimu Afrika Instagram, Facebook, Twitter, YouTube na www.elimuafrikatz.blogspot.com #SiasaIsiingilieTaaluma.

0 Comments