DAWASCO WATOA ELIMU


Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro akitoa elimu juu ya matumizi ya mfumo wa DAWASCO kwa kwa njia ya simu kwa watumiaji wa vyombo vya Moto hususani Bajaj na Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam. Mfumo huo umezinduliwa rasmi ili kutoa nafasi kwa wananchi kupata na kutoa taarifa sahihi za DAWASCO.

Mmoja ya waendesha bodaboda akimuuliza swali Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWSCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa.

Mwendesha bajaji akihojiwana ITV juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWASCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa.

Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.

“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.

Amesema kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO.

0 Comments