UTOVU WA NIDHAMU KWA WANAFUNZI NI CHANGAMOTO INAYOKABILI TAIFA

Arusha Mjini: Huyu ni mmoja wa Mwanafunzi aliyekamatwa na walimu kwenye pango alipokuwa amejificha akitumia bangi. Mwanafunzi huyu anasoma kidato cha pili kwenye shule ya sekondari Arusha Mjini.

Baadhi ya wanafunzi wamekuwa na tabia ya kuondoka nyumbani badala ya kwenda darasani huwenda kujificha kwenye mapango wakitumia miadarati hasa Bangi. Lazima wazazi wachukue hatua kuwafuatilia watoto wao kama wanafika shuleni na kukagua maendeleo yao yakitaaluma na kinidhamu.

Jamii imekuwa ikishusha lawama, dharau na kejeli nyingi kwa walimu kama sababu ya wanafunzi kufeli,  ila nadhani jamii ibadili mtazamo kwa kuangalia hali halisi walimu changamoto wanazokabiliana nazo.

0 Comments