WALIMU WAPEWA MAFUNZO YA WIKI MOJA YA KOMPYUTA



Kwa ufupi

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu asubuhi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete wakati akifungua mafunzo ya wiki moja ya walimu nchini.

 Serikali imeanza kutoa mafunzo kwa walimu nchini jinsi ya kutumia kompyuta na kutatua matatizo madogo baada ya mafundi kutumia mwanya huo kujipatia fedha kwa njia za ujanja ujanja.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu asubuhi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete wakati akifungua mafunzo ya wiki moja ya walimu nchini.

Amesema mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yanalenga katika kuondoa changamoto hiyo na kuongeza ufanisi katika ufundishaji shuleni.

"Kuna wajanja wachache wamekuwa wakitumia mwanya wa kutokuwa na uelewa wa mambo ya tahama kujipatia fedha lakini kwa mafunzo haya yatawasaidia kuondoa changamoto hizo," amesema.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Pauline Nkwama jumla ya walimu 309 kutoka shule mbalimbali nchini watanufaika na mafunzo hayo ya wiki nzima ambapo watajifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Tehama

0 Comments