WANAFUNZI KADHAA WAFARIKI KWENYE AJALI- MOROGORO


Watu tatu wamefariki Dunia huku wengine 28 wakijeruhiwa, baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria kugonga Treni ya abiria katika eneo la Tanesco Manispaa ya Morogoro, huku idadi hiyo ya Majeruhi wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa Shule za Sekondari Tushikamane, na Mji Mpya.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja na nusu asubuhi ikihusisha Daladala lenye namba za usajili T 438 ABR na ilikuwa imebeba Abiria 31, huku wakiwamo wananfunzi hao ambao walikuwa wakielekea shuleni.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa daladala hiyo, ambaye alijaribu kulazimisha kuvuka kwenye kivuko cha Treni kilichopo katika eneo hilo, licha ya kupewa ishara ya ujio wa Treni hiyo ya Abiria iliyokuwa ikitokea Kigoma, na ilipofika katikati, daladala hiyo ilizima na kugonga upande wa ubavu na kupelekea vifo hivyo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogor Dr Jacob Frank, amekiri kutokea kwa vifo hivyo na kupokea majeruhi 28, ambao wanaendelea kupatiwa Matibabu katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo Dereva wa Daladala hiyo alijaribu kutoroka, hata hivyo wananchi walifanikiwa kumkata na kumshushia kipigo, kilichompatia majeraha kadhaa, ambapo alikimbizwa katika Hospital hiyo kwa matibabu zaidi.

0 Comments