TCRA YATOA ELIMU KWA WAMILIKI VYOMBO VYA HABARI MITANDAONI.


Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Jones Kilimbe

Na. Daniel, Dar es salaam

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania imefanya semina ya nusu siku na wamiliki wa mitandao ya kijamii leo jijini Dar es salaam ikiwa na lengo la kuangalia matumizi bora ya mitandao ya kijamii

Akizunguza katika ufunguzi wa semina hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA Jones Kilimbe amesema kuwa mawasiliano yamepiga hatua hadi sasa zipo Luninga za mtandaoni zipo zaidi ya 50 ambapo Luninga za kawaida zipo 35 Watoa habari kwa njia ya mtandaoni wapo zaidi ya 150.

Amesema kuwa Mamlaka ya mawasiliano inalo jukumu la kuimarisha na kusimamia vyema habari za mitandaoni ili kuleta ufanisi zaidi kwani mitandao hiyo ikitumiwa vibaya inaweza kuketa madhara katika jamii

Ndugu Kilimbe amesema kuwa teknolojia hii imekuwa kwa kasi kubwa kwani taarifa zinapatikana kwa haraka zaidi kwa simu ya mkononi zaidi ya TV na Radio, hivyo mitandao itumike vizuri kwa mustakabali wa Taifa ,kwani jamii inapokea  habari na kusambaa  kwa haraka zaidi.

Mara baada ya ufunguzi walialikwa watoa mada ambao kwa ujumla wao  Mosi matumizi salama ya mitandao ya kijamii, wawasilishajimada wote walisisitiza uzalendo na maadili ya uandishi wa habari zetu na kuhariri vema kabla ya kuzirusha ili kuepuka usumbufu wowote kwa wasomaji.

Pili maudhui ya mitandaoni, faida na changamoto zake, kimsingi maudhui yawe ya kulinda, kutunza na kukienzi kiswahili kama lugha ya Taifa, ili kukuza lugha hii kuwa yakimataifa lazima vyombo ya habari mitandaoni kuzingatia usanifu katika habari zao.

Tatu tulielezwa na mwakilishi wa Jeshi la Polisi kitengo cha ualifu mitandaoni kuwa  hali ya usalama mitandaoni ni nzuri na wamesisitiza kuwa kila mara hufanya doria kwenye kurasa mbalimbali ili kuhakikisha hali nzuri ya usalama bila kuingilia uhuru binafsi wa mawasiliano ya mtu.

Nne Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imezindua kampeni ya uelimishaji umma kuhusu matumizi bora ya mitandao ya kijamii awamu ya pili. Ambayo Elimu Afrika itairusha moja kwa moja kupitia kurasa zetu zote za mitandao ya kijamii.

Mafunzo hayo ni moja ya jukumu lao la msingi na ni muendelezo wa kampeni za matumizi salama ya habari za mitandaoni

Hatahivyo Elimu Afrika ilipata fursa yakuchangia, ilisisitiza TCRA kuja na kampeni na mambo mengine chanya ya kuwezesha wamiliki wa vyombo vya habari mitandaoni wanashindana katika mambo chanya, badala ya kutengeneza mazingira hasi yatakayosababisha waandishi kujikita kuzungumzia mambo hasi badala ya chanya.

Pia tulisisitiza uanzishaji au uboreshaji wa tuzo mbalimbali kwa vyombo vya habari mitandaoni ili kuhakikisha wanahabari wanashindana kuandika na kurusha mambo chanya, yakizalendo na kuelimisha na kujenga taifa moja lenye ushirikiano katika habari nzuri.

Tumewaomba wanahabari wenzetu kuacha tabia ya kuthamini fedha au biashara kwa kurusha habari za aibu zisizo za kiadilifu kwa kupewa fedha au kusaka umaarufu wa watazamaji badala yake wanahabari kujali Utu zaidi katika kuwahabarisha watanzania.

Mwisho tunashukuru sana TCRA kutualika kwenye warsha hii, tukipendekeza warsha zijazo ziwe za majadiliano yasiyorasmi (informal dialogue / discussions). Tunawapongeza sana TCRA kwa kuendelea na jitihada za uelimishaji, usimamizi na uongozaji bora wa mawasiliano Tanzania.

0 Comments