CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Simanjiro mkoani Manyara, kimewakabidhi walimu 10 wastaafu Sh milioni 3.4 kwa ajili ya ununuzi wa mabati 200.
Mwenyekiti wa CWT wilayani Simanjiro, Abraham Kisimbi aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mji mdogo wa Orkesumet. Mwalimu Kisimbi wamewapa walimu hao wastaafu 10 fedha hizo kuwawezesha kupata jumla ya mabati 200 ambapo kila mmoja atapata mabati 20 yatakayowasaidia kuezeka nyumba zao watakazojenga na kuanza maisha yao ya ustaafu.
“Tumeona badala ya kuwapa mabati na kuhangaika kusafirisha kila mmoja tumempa hundi ya Sh 340,000 ili akanunue mabati 20 kule anapoishi,” alisema mwalimu Kisimbi. Aliwataka walimu hao kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyopangwa ili wakafanikishe maisha yao kipindi hiki ambacho watakuwa wamestaafu kazi zao za ualimu na kuanza maisha mengine.
Mwalimu Nazama Tarimo akisoma risala ya CWT alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo walimu kutopandishwa madaraja, kutolipwa madai yao, kutembea umbali mrefu na msongamano wa wanafunzi madarasani kunasababisha walimu kushindwa kufikia asilimia 80 ya ufaulu kwa wanafunzi wa eneo hilo.
Mwalimu mstaafu Peter Toima ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT alisema kwa kutambua thamani ya elimu ameiunga mkono serikali kwa kukarabati, kukarafati na kujenga madarasa mapya kwenye shule mbalimbali
0 Comments