Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mara kupitia Catherine Ruge amekabidhi Sare za Shule kwa Wanafunzi zaidi ya 413 kutoka Shule za Msingi zipatazo 10 Wilayani Serengeti Mkoani Mara ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wake wa kusaidia sekta ya elimu wilayani humo, huku akisindikizwa na viongozi mbalimbali wilayani hapo pamoja na walimu kutoka shule zilizotoa wanufaika.
"Najisikia furaha kubwa sana leo ninapochangia maendeleo ya watoto wetu wa Serengeti kufikia ndoto za maisha yao kupitia elimu." Alisema Mbunge Catherine
Catherine amesema pamoja na kutambua thamani na umuhimu wa elimu unaomfanya kuelekeza nguvu zake zaidi katika sekta hiyo lakini kwa kufanya hivyo pia anatimiza kwa vitendo ahadi ya Chadema ya kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu.
Aidha amewashukuru watu na Taasisi mbalimbali zilizomuunga mkono katika kampeni yake hiyo ambayo inalenga kuwajengea mazingira mazuri ya masomo watoto hasa wanaotoka katika kaya masikini na wanaoishi katika mazingira ya vijijini.
Nikiwa Mama ninaetoka Serengeti hii kwangu ni heshima kubwa kuitumia nafasi yangu ya Ubunge kuboresha maisha ya wanaSerengeti wenzangu."
Wanafunzi hao ambao wametoka katika kaya masikini na yatima wamenufaika na msaada huo huku wakimshukuru Mbunge huyo kwa kuwapatia sare za shule na hivyo kuwafanya wafanane na Mwanafunzi wenzao mashuleni.
Mbali na msaada huo wa sare za shule Mbunge Catherine alitembelea bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Ring'wani alilojenga kupitia taasisi ya GIRLS EDUCATION SUPPORT INITIATIVES (GESI) ambayo yeye ni mmoja wa waanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, yenye makao yake makuu Mugumu mjini.
Catherine alipata fursa pia ya kusikiliza changamoto mbalimbali toka kwa uongozi wa shule alizotembelea na kuahidi kushirikiana na wananchi kuzitatua ikiwa ni kuenzi na kuthamini wajibu alioaminiwa na chama chake na wananchi katika nafasi yake ya Ubunge.
Imeandaliwa na Katibu wa Mbunge.
0 Comments