MISAADA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI WATOKEWA


Mwanzilishi wa Taasisi ya Albinism Awareness Foundation Bw. Suleiman Magoma akizungumza na wanahabari wakati wa hafla hiyo.

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mohamed Al Amir akiteta na wanahabari wakati wa hafla ya utoaji misaada katika Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu.

Mkurugenzi wa Shule akieleza jambo kwa Mhe. Hassan Al Amir Kaimu Balozi wa Kuwait, na Bw. Suleiman Magoma, Mwanzilishi wa Taasisi ya Albinism Awareness Foundation

Watoto wenye ulemavu walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.


Taasisi ya Albinism Awareness Foundation kwa Kushirikiana na Ubalozi wa Kuwait Nchini jana tarehe 13 Februari 2017 walifanya ziara katika Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu na kutoa misaada ya vifaa mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu (wakiwemo wenye uao) wanaosoma na kulelewa katika shule hiyo.

Aidha hafla hiyo ilihudhuliwa na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salam Bw. Khamis Lissu aliyewakilishwa na Afisa Elimu Taaluma Mkoa, Bibi Given Sure, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa, Bw. Gabriel Aluga, Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulbino(TAS) Mkoa wa Dar es salaam, wageni mbalimbali pamoja na waandishi wa habari

Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Kofia, Miwani ya jua, Telescope kwa ajili ya kukuzia maandishi,mafuta maalum ya kukinga ngozi dhidi ya mionzi ya jua(sunscreen lotion),Wheel chairs, working stick,stick for blind,crutches elbow type na crutches ampith kwa ajili ya watu wenye ualbino, wasioona na wenye ulemavu wa viungo.

Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi jeshi la Wokovu, Mwanzilishi wa taasisi ya kuongeeza uelewa kwa jamii dhidi ya Watu wenye Ualbino(Albinism Awareness Foundation) Bw. Suleiman Magoma aliushkuru Ubalozi wa Kuwait nchini kwa imani kubwa waliyonayo dhidi ya taasisi hiyo na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya watu wenye ulemavu(wakiwemo wenye ualbino).

Naye Kaimu Balozi wa Kuwait nchini Bw. Mohamed Al Amir alieleza kuwa Serikali ya Kuwait inatambua umuhimu wa kusaidia Watu wenye ulemavu na kwamba Ubalozi umetenga kiasi cha zaid ya dola za marekani 500,000/= ili kusaidia watu wenye ulemavu.

Albinism Awareness Foundation (AAF); ni Shirika lisilo la Kiserikali lililoanzishwa chini ya sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Na. 24 ya mwaka 2002, linalojishughulisha na utetezi wa haki za watu wenye ualbino kwa kuhakikisha elimu ya kuongeza uelewa dhidi ya watu wenye ualbino inaifikia jamii na hivyo kuachana na vitendo vya ukatili,unyanyapaa na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino nchini Tanzania

Wanafunzi wa Shule ya Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu walishkuru taasisi ya Albinism Awareness Foundation pamoja na Ubalozi wa Kuwait kwa kuwapatia misaada hiyo na kutoa wito kwa taasisi mbalimbali na wadau wa maendeleo kusaidia watu wenye ulemavu nchini.

0 Comments