Wanafunzi wakipata chakula cha mchana.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo akishiriki uchimbaji wa mtaro wa kutandaza mabomba. Waliopo nyuma yake ni Mhe. Maneno Diwani wa Chakwale na Mtendaji Kata ya Chakwale
Mhe. Mchembe akiongea na wananchi kuhamasisha umaliziaji wa madarasa 5 shule shikizi ya Iringa.
Diwani wa Kata ya Mangapi Mhe. Maneno akiongea na wananchi. Waalimu wa mazoezi wote wa shule shikizi wanaishi nyumbani kwa Diwani kama familia.
Chakula kwa wanafunzi ni cha muhimu sana kwani kinawapa nguvu, utulivu na umakini mkubwa wanafunzi hivyo kuongeza Ufaulu.
Hayo yamesemwa siku ya leo Aprili 22, 2018 na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe mara baada ya kutembelea baadhi ya shule Kata ya Kibedya na Chakwale.
Ziara hiyo ameifanya leo akishirikiana na madiwani wa kata hizo, ya Kibedya ikiongozwa na Mhe. Mangapi na Chakwale ya Mhe. Maneno huku mkuu huyo wa wilaya akiwapongeza kwa kusimamia vizuri zoezi la kuhakikisha chakula hakikosekani katika shule zao.
"Napenda kuwashukuru wazazi kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wenu wanasoma katika mazingira mazuri, tuendelee kushirikiana ili matokea yawe chanya," amesema Mhe. Mchembe.
Katika ziara hiyo Mhe. Mchembe alishiriki uchimbaji mtaro wa kutandaza mabomba ya maji Kata ya Chakwale, mradi unafadhiliwa na Lions Club ambao mpaka sasa umewezesha upatikanaji wa maji Kata ya Chakwale kutoka asilimia 35 hadi 72.
Mhe. Mchembe ametoa shukurani zake kwa Lion's Club kwa kazi kubwa wanayofanya Gairo katika kutatua changamoto ya maji.
Mwisho Mhe. Mchembe alifanya mkutano na wazazi shule shikizi ya Iringa ambapo ndani ya mwezi mitano wanategemea kumaliza madarasa matano ambapo matatu yapo ngazi ya boma na mawili bado ni msingi. Vifaa vya kumalizia vimepatikana pia amechangia mifuko 50 ya saruji.
Baada ya mkutano alishiriki kugawa chakula aina ya makande kwa wanafunzi wa Kibedya Shule ya Msingi.
0 Comments