ELIMU KUHUSU LUGHA YA ALAMA KWENYE KONGAMANO LA ELIMU, ARUSHA

Bi. Linda Malisa Afisa Elimu Maalum, Elimu Afrika. akielimisha kuhusu umuhimu wa lugha ya alama kwenye jamii. Bi Linda Malisa ameeleza kuwa lugha ya alama husaidia watu kuweza kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kusikia.

Ni kama burudani, huokoa muda, huleta usawa katika jamii, humuwezesha mlemavu kufanya kazi zao kwa ufasaha na kushiriki vyema katika shughuli za kulijenga Taifa.


Hivyo ameitaka jamii na walezi kujifunza lugha ya alama na kuwapeleka shule watu wenye ulemavu wa kusikia na kuto waficha ili kujenga usawa wa haki kwa walemavu.
 Mwanzilishi na Mkurugenzi Elimu Afrika akifurahia jambo na mwalimu Ewald Mallya ambaye anausikivu hafifu.
 Mwanzilishi na Mkurugenzi Elimu Afrika Mwalimu Daniel Urioh katika picha na walimu wa Elimu Maalum Nossim Aloyce, Linda Malisa na Ewald Mallya .

0 Comments