Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika Mwl. Daniel Urioh.
Akizungumza kwenye Kongamano la Elimu, lililokuwa na maudhui ya Kuandika Historia Chanya ya Elimu Yetu.
Taasisi binafsi inayojihusisha na maswala ya elimu nchini Tanzania,leo tarehe 24.3.2018 imefanya Kongamano lake la elimu katika ukumbi wa shule ya msingi Arusha ambapo washiriki walielimishwa mambo mbalimbali yakielimu ikiwemo elimu ya Bima ya Afya, Usalama barabarani, Sera ya elimu 2014, Ushauri wakitaalamu na lugha ya alama.
Mgeni Rasmi Prof. Raymond Mosha.
Kwa upande wake Mgeni rasmi amesema elimu inayowafaa wananchi ni elimu ambayo inamisingi na maadili na usawa ndani yake kwani itamjenga msomaji kimaadili na kiuadilifu.
Pia amewataka wasomi watumie elimu yao kuwasaidia watu wengine katika kuwapa elimu ili kuinua sekta hiyo ya elimu kwa maendeleo ya nchi.
Wageni waliohudhuria mkutano wa Elimu Afrika wakiwemo wanafunzi na wadau wa elimu nchini.
Koplo Athilio Choga, Kitengo cha Uelimishaji Jamii Trafiki Mkoa wa Arusha.
Koplo Athilio Choga amewataka watumiaji wa barabara kuheshimu sheria zilizowekwa na mamlaka ya usalama barabarani ili kuepuka ajali za barabarani.
Hatahivyo amesema ajali nyingi zinazo tokea babararani husababishwa na ukaidi wawatu kuto kuheshimu sheria hizo ,jambo ambalo ni changamoto katika kuzuia ajali hizo.
Pia amesema kwa upande wa baadhi ya wanawake wamekuwa wakikaidi kuvaa kofia ngumu wakihofia kuharibu nywele, mawigi na mapambo mbalimbali.
Mkurugengi wa Kismaty Advert Media Co. Ltd Madam Mary Mollel
Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya utoaji wa habari na matangazo Kismaty Advert Media Madam Mary Mollel ameeleza faida ya uwepo wa vyombo vya habari nchini hususani uwepo wa mitandao ya kijamii unavyo saidia kuboresha na kukuza sekta ya mawasiliano nchini. Ikiwemo kuhabarisha umma, kukosoa, kuelimisha, kukuza lugha na kuimarisha amani
Mfanyakazi wa Kismaty Advert Media, Nickson Sawe
Sambamba na hayo mfanyakazi wa kampuni hiyo Nickson Sawe ameelezea faida ya kuwa na elimu ya uandishi wa habari ili kumfanya mwandishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
Na kueleza wapo baadhi ya watu ambao hawana elimu ya kutosha juu ya uandishi wa habariambao hushusha thamani na hadhi ya tasnia hiyo hapa nchini.
Mwalimu wa lugha ya Alama na Afisa Elimu wa Taasisi ya Elimu Afrika Bi. Linda Malisa
Katika kongamano hilo mwalimu wa lugha ya Alama kwa walemavu wasiosikia Bi Linda Malisa ameeleza faida ya lugha ya alama husaidia watu kuweza kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kusikia.
Nakuezeza faida ya lugha hii husaidia kuburudisha, kuokoa muda,kuleta usawa katika jamii kumuwezesha mlemavu kufanya kazi zake kwa ufasaha na kushiriki vyema katika shughuli za kulijenga taifa.
Hivyo ameitaka jamii na walezi kujifunza lugha ya alama na kuwapeleka shule watu wenye ulemavu wa kusikia na kuto waficha ili kujenga usawa wa haki kwa walemavu.
Pia ameeleza lugha hii hutumia viungo vya mwili wa binadamu kuanzia kitovuni kuelekea juu.
Dokta Nguma mdau wa elimu na mjasiriamali
Kwa upande wake amesema utoaji wa elimu ni muhimu kwa kizazi kijacho kwani ndiyo urithi pekee unaodumu. Pia amesema elimu ya Afrika haina hadhi ya kiafrika nahii ni kutokana na kurithi elimu kutoka kwa wazungu na watu husoma kwa kuwa wamepata fursa ya kusoma lakini wanachokisomea sio kipaji chao jambo ambalo wapo wasomi wengi katika Afrika lakini hakuna maendeleo.
Elimu Afrika imekuwa ikitoa elimu kwa umma kupitia Vyombo vya habari Mtandaoni (OnlineMedia), kwa kuandaa vipindi mbalimbali vya elimu, hivyo kongamano hili ni sehemu ya kupata vipindi vya kurusha.
Dhumuni kuu la Kongamano lilikuwa kupata maoni ya wadau wa elimu ili kuandika Kitabu cha "Historia Chanya ya Elimu Yetu" hivyo wadau mbalimbali wa elimu walikutana kuhabarishana, kuelimishana na kujadiliana kila mmoja kwa ubobezi wake.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbali mbali wa Elimu, yaani walimu, waandishi wa vitabu, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na viongozi wa taasisi mbalimbali ambao wote walishiriki katika mada za elimu.
0 Comments