KWANINI WANAFUNZI WA CHUO KIKUU KENYA HUJIUNGA NA MAKUNDI YA UGAIDI?

Serikali ya Kenya inasema zaidi ya wanafunzi 58 wa chuo kikuu waliamua kuachana na masomo na kujiunga na makundi ya kigaidi. Wengi walisajiliwa katika makundi ya wapiganaji nchini Somalia, Libya na Syria. Ripoti ya serikali ambayo imefichuka inasema baadhi ya wanafunzi walikamatwa na maafisa wa usalama wakati wakijaribu kukimbia.

Mwenda Njoka, msemaji wa wizara ya usalama wa ndani nchini Kenya ameielezea BBC imekuwaje wanafunzi hawa kuondoka na kujiunga na makundi ya kigaidi bila maafisa wa ujasusi kufahamu?

0 Comments