Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amehoji wanafunzi wa chuo cha Mkwawa iwapo kujua kusoma ni kujua Kiingereza.
Rais Magufuli ameyasema hayo jana , Mei 2 wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa wakati akitoa ufafanuzi wa shule za private na shule za Sekondari.
''Eti mtu amemaliza form four halafu hajui kuandika barua ya Kingereza, kwani kusoma ni kujua Kingereza!? Warusi wanajua Kingereza!? Kwani Wachina wanajua Kingereza !? Mbona wanatengeneza silaha za kila aina" !?

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa “Shule za private wanafunzi wake wanachujwa, wakifika form 2 kuingia form 3 wanawachuja tena. Wanabaki na ile cream ili waonekane wanaongoza. Serikali inayowapenda wananchi wake haiwezi ikafanya hivyo.”
0 Comments