Naibu Waziri Wa Kazi Ajira Na Vijana Mheshimiwa Anthony Mavunde Akigawa Maziwa Ya Asas Kwa Wanafunzi Waliojitokeza Kwenye Viwanja Vya Nyerere Square jijini Dodoma Kwenye Kilele Cha Unywaji Wa Maziwa Duniani ambapo Kitaifa Imeadhimishwa Mkoani Arusha
Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Nkuhungu Ya jijini Dodoma Wakigawiwa Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD.
Wanafunzi Wa Shule Ya Nkuhungu Wakifurahia Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD
Naibu Waziri Wa Tamisemi Mheshimiwa Josphat Kandege Na Mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Mh. Mrisho Gambo Wakipokea Maziwa Kutoka Kwa Mwakilishi Wa Asas Dairies Lipita Mtimila Kwa ajili Ya Shule Za Mkoa wa Arusha Ambapo ASAS DAIRIES LTD Wametoa Maziwa pakiti 15,000 Kwa Wanafunzi wa mkoa huo.
Naibu Waziri Wa Tamisemi Mheshimiwa Josphat Kandege Akisaini Kitabu Cha Wageni Alipotembelea Banda La ASAS DAIRIES LTD Kwenye Madhimisho Wa Wiki Ya Maziwa Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Arusha.
Mheshimiwa Richard Kasesela Akuu wa Wilaya ya Iringa Na Mkurugenzi Wa ASAS DAIRIES LTD Ahmed Salim Asas wakiwa Kwenye Viwanja Vya Ngombe Mjini Iringa Kwenye Kilele Cha Madhimisho Ya Wiki Ya Maziwa Duniani.
Wanafunzi Wa Shule Ya Kihesa Ngombe Wakifurahia Maziwa Ya ASAS DAIRIES LTD wakati Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesela na Mkurugenzi wa ASAS DAIRIES LTD Bw. Ahmed Salim Asas walipokuwa wakiwagawia.
Mheshimiwa Kasesela Akimpatia Maziwa Mmoja wa Mwanafunzi Wa Shule Ya Kihesa Ngome mjini Iringa.
---
ASAS DAIRIES LTD imegawa zaidi ya pakiti 400,000 kwenye shule mbalimbali za mikoa ya IRINGA, ARUSHA, MBEYA na DODOMA. wakati wa maadhimisho ya wiki ya Maziwa duniani ambapo kitaifa inafanyika mkoani Arusha.
ASAS DAIRIES LTD ilianza kampeni hii Tarehe 22 mwezi wa Tano na kufikia zaidi ya shule 108 na Wanafunzi 67,000. Hii inatokana na uhamasishaji wa unywaji wa Maziwa Mashuleni ambao unafanywa na ASAS DAIRIES LTD kila mwaka.
Katika kufikia lengo la watanzania kunywa maziwa kwa wingi kampuni ya ASAS DAIRIES LTD imejikita katika kampeni hiyo ili kuwafanya watoto ambao
watakuwa wazazi wa baadaye kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya zao pamoja na vizazi vyao kwa siku za baadaye.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha ASAS DAIRIES LTD Bw. Amded Salim Asas amesema huu ni mwendelezo wa kampeni hiyo na lengo la kampuni hiyo kwa mwakani ni kuzifikia shule za msingi nchi nzima, Bw. Ahmed Asas ameishukuru
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa ngazi zote jinsi ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa kwao na kuifanya ndoto ya Tanzania ya Viwanda kwenda kutimia kwa mafanikio makubwa.
0 Comments