NECTA YAVIFUTIA USAJILI VYUO 20




Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) limetangaza kuvifutia usajili vyuo 20, baada ya kushindwa kufuata sheria zinazoendana na matakwa ya usajili wa vyuo hivyo.

Dk Adolf Rutayuga Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, ametangaza uamuzi huo na kusema umefikiwa baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa vyuo 458 na vyuo 32 vimekutwa na mapungufu.

Amesema pamoja na vyuo 20 vilivyofungiwa, vyuo tisa vimezuiliwa kudahili wanafunzi wapya huku vyuo vitatu vikitakiwa kusitisha baadhi ya kozi zilizokuwa zikitolewa bila idhini ya baraza.

Dk Rutayuga amesema tayari baraza hilo limeshaviandikia barua vyuo 20 vilivyofungiwa, kuvitaka vihakikishe wanafunzi wanahamia kwenye vyuo vingine.

Vyuo vya Dar es Salaam vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Royal College, Covenant College of Business Studies, Mugerezi Spatial Technology College, Techno Brain, Lisbon Business College, PCTL Training Institute na Mlimani School of Professional Studies.

Vingine ni Regency School of Hygiene, St Peters College of Health Sciences, Genesis Institute of Social Science, Institute of Management and Information Technology na Boston City Campus of Business College, Arusha Institute of Technology, East African Institute of Enteprenuership and Financial Management (Arusha) Iringa RETCO Business College (Iringa) na Musoma Utalii College (Musoma), Highlands Health Institute (Njombe), Institute of Social Work na Dinobb Institute of Science and Business Technology (Mbeya).

0 Comments