VIONGOZI
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Morogoro, wanatuhumiwa kuwatishia Walimu
wanaoonekana ni Wafuasi wa Chama cha CHADEMA, ambapo miongozi mwa Walimu
wenye Vyeo, wanadaiwa kutumika kuwafuatafuata katika maeneo yao ya
kazi, ili Ajira zao zisitishwe.
Hayo
yamebainika katika Makundi ya Viongozi wa CCM wa Wilaya mkoani
Morogoro, waliomdokeza Mwandishi wetu kwamba, kutokana na Walimu hao
kutishia uwepo wa baadhi ya Wabunge katika Majimbo yao mwaka 2015,
Wameamua kuwatishia Nyau Walimu hao.
Walimu
Wanne wa Wilaya za Mvomero, Kilosa, Gairo na Kongwa inasemekana tayari
wameonja Joto hiyo ya Jiwe, ambapo mmoja wao ameapa akisema, Iwapo wana
siasa Uchwara na Mbunge mmoja anayekataliwa na wananchi atathubutu
kumfuata, atamburuza mahakamani.
“Ni
kweli mimi ni mmoja wa ambao nimeandikiwa barua na Mwalimu wangu Mkuu
Msaidizi, kwamba nimekuwa nikionekana kwenye mikutano ya Chadema, hivyo
natakiwa nijieleze kwa maandishi, ili nisichukuliwe hatua za kinidhamu.
“Binafsi
sina Mashaka, kwa sababu najua hakuna Mzazi anayeweza kumchagulia
Mwanae Mume au Mke wa kuishi naye isipokuwa wenzi wenyewe, hivyo
nangojea tishio hilo la Nyau linifikie ili name nitoe majibu”.alisema
Mwalimu huyo aliyeomba asitajwe jina lake.
Walimu
hao walisema, wanataka kuunganisha Nguvu kuweka Mawakili Sita makini
nchini watakaowatetea kwa umoja wao, pindi ujinga huo utakapoibuliwa na
kuwa Kesi, ili warumbane kisheria mahakamani, kama ipo Sheria ya
kumlazimisha mtu kupenda Chama asichokitaka.
Aidha
mmoja wa wanasheria maarufu wa kujitegemea mkoani Morogoro ambaye
hakutaka jina lake litajwe alisema, “Hakuna Sheria inayomlazimisha mtu
kupenda kitu asichokipenda, hivyo kitendo kinachofanywa na wanasiasa hao
kinakiuka hakiza Binadamu kwa faida yake.
0 Comments