MH. NAIBU MEYA APIGWA NA KUUMIZWA VIBAYA NA MGAMBO WA JIJI LA ARUSHA


Mh Naibu Meya wa Jiji la Arusha Prosper Msoffe akimeza Dawa baada ya kipigo kikali toka kwa Mgambo wa Jiji la Arusha

Mh. Naibu Meya Prosper Msoffe ameeleza kiini cha tatizo kuwa yeye kama kiongozi wa wananchi amekuwa akipokea malalamiko mengi ya wananchi kupigwa, wengine kuvunjwa miguu, mali kuporwa na mgambo, mali kifadhiwa depoti hadi kuoza. Hivyo akaamua kufika eneo la depoti leo kujionea hali halisi na kuzungumza na mgambo na wananchi, baada ya kufika eneo la tukio Alianza kushambuliwa kwa virungu na mateke, huku wakisema wewe umekuwa kiherehere sana na mtetezi wa wananchi sasa tunakukomesha. 

Mh. Naibu Meya alishangazwa pia kuona kiongozi mwenzake Diwani wa Levolosi kufika pale nae akapigwa kwelikweli, "jambo hili tunalilaani sana na tunawataka vijana hao waliotekeleza shambulizi hili kuchukuliwa hatua za kisheria" Alisema Mh Naibu Meya. 

Kadi ya matibabu ya Kituo cha Afya Levolosi, ikionyesha Mh. Naibu Meya Kumetibiwa na kuandikiwa dawa.

Wananchi na Wanachama wa Chadema Wakiwa nje ya Geti la deboti ya Jiji na Kituo cha Afya cha Levolosi wakisubiri hatma ya Viongozi wao.

Hakuna Kulala Mpaka kieleweke

Hakuna Kulala Mpaka kieleweke

Hakuna Kulala Mpaka kieleweke

Hakuna Kulala Mpaka kieleweke




0 Comments