KIWANDA CHA (A TO Z) KINA HATARISHA MAISHA YETU OLASITI


Wananchi Waliazimia
Wananchi walipokaa kikao tumeazimia tukague ukweli na madhara yaliyosababishwa na maji haya, wananchi walimeamua kwenda mguu kwa mguu kukagua maji hayo, eneo lililotengwa na Kiwanda kutitishiwa uchafu wote wa kiwanda, hata hivyo eneo lenyewe ni la wazi sana, ukuta umeanguka, bwawa la maji machafu halijawekwa kulingana na Maelekezo ya Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).
“Tumekagua tumejiridhisha kuwa mwekezaji huyu ni Adui wa Mazingira, Afya na Wakazi wa Olasiti, kwasababu kwa jinsi alivyojenga miundombinu yake ya majitaka na taka za kiwanda ina dhihirisha kuwa alidhamiria kufanya hivi”
Azimio la Kikao na Matembezi ya Ukaguzi wa Madhara yanayosababishwa na maji taka ya kiwandani yatafuata baada ya kwenda kujadiliana katika kikao cha mitaa au kata ya Olasiti kwa Ujumla kwasababu ndio wanaoathiriwa na tatizo hili, kikao kitaamua cha kufanya.
Add caption

Wananchi Wakikagua kwa Umakini mkubwa ili kuridhika kuwa kweli Maji yale yanatokea kiwandani na ni Machafu yenye rangi ya sumu
Maji yakikatiza kwenye moja ya barabar ya Oloresho

Kweli hawajamaa ni katili kweli, Wananchi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa na Balozi wakijiaminisha

Kinachonisikitisha kabisa nimekuwa nikizungumza kuhusu jambo hili kwenye kikao cha maendeleo ya Kata ambayo mwenyekiti wake ni Diwani, ila kweli Diwani hajaonyesha nia ya dhati yakutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili”
Hatahivyo mkt anashangazwa kuwa
“Ninashangaa zaidi kuwa viongozi wa mtaa wa Mateves wamefumbia majo jambo hili, afisa mtendaji anatambu ila wako kimya, wakazi wa mateves, wenye mashamba haya ambapo maji yanakatisha na yameshakuwa kama Mto wako kimya, maji haya yanaonekana kuwa na sumu, yanatoa harufu mbaya, kiasi cha kuchafua mazingira kwa harufu, kutiririka bila kusahau kuhatarisha afya ya wakazi, zaidi sana watoto ambao hawajitambui wamekuwa wkicheza kwenye mto huu wenye maji machafu”

Akizungumza kwa uchungu mwananchi John Laizer wa Mtaa wa Mateves, alisema tulisha andika barua kwenye ofisi ya mtaa na wilaya kueleza kuhusu shida ya kiafya inayosababishwa na Kiwanda cha (A to Z)
“Yaani mimi nashukuru kuwaona wakazi wenzangu wa mtaa wa Oloresho, sisi tumejaribu kupambana na tatizo hili lakini viongozi wetu ni Bure kabisa, mwenyekiti wa mtaa hana lolote, Diwani ndie kabisa hatutetei kabisa sisi tunaathiriwa na Arufu mbaya ya maji taka, maji hayo yamearibu mashamba yetu, daraja limearibika hata mtu ukitaka kutumia Gari kumpeleka mgonjwa kwa sasa ni shida kabisa huwezi kwsababu barabara imearibiwa” alisema John Laizer wa mtaa wa Mateves.
Hatuta lala Mpaka kieleweke
Balozi nae alisema
Balozi Ndugu Aminiel John ameonyesha nae kusikitishwa na tatizo hili sugu “ndugu yangu mi ninasikitika kwasababu eneo la Mateves ambapo kiwanda kipo na kimejenga miundombinu mibovu ya maji taka viongozi wapo, ofisi ya mtaa ipi, Diwani ni jirani na hapa wote wamefumbia macho ufedhuli huu”

0 Comments