KIWANDA CHA (A TO Z) HATARI KWA MAZINGIRA NA AFYA YA WAKAZI WA OLASITI

Nikiwa na wakazi wenzangu wa Kata ya Olasiti, Mtaa wa Oloresho, tukikagua ili kujiridhisha kuwa mwekezaji wa (A to Z) ameelekeza mfumo wa Maji taka wa Kiwanda chake kwenye chanzo cha Maji cha Mto Oloresho. Katika picha tukitizama ukuta ulioanguka kutokana na maji taka hayo kuathiri msingi wa Ukuta wa A to Z.


“Namimi ni Mwananchi wa Olasiti, mdau wa Mazingira, Elimu na Afya, nimesikitishwa sana na Mwekezaji huyu wa (A to Z) kutupuuza na kutudharau kiasi hiki, kimsingi ninalaani jambo hili kwasababu ina hatarisha Uhai wa Viumbe, wanyama na binaadamu kwa ujumla. Nasikitishwa pia na Udhaifu ulio na unao onyeshwa na Viongozi walipewa dhamana yakuwatumikiwa wananchi wa Olasiti kutotekeleza matakwa ya Wananchi”
Ninashauri Wananchi wa Olasiti, hasa wa mtaa wa Mateves na Oloresho kutambua kuwa kwasasa njia pekee iliyosalia ni kutumia “Nguvu ya Umma ili kupata Ufumbuzi wa Kudumu wa Tatizo hili”


Mwenyekiti wa Mtaa wa Oloresho, Ndugu. Eliakimu Olodi akieleza Sakata lote alianza
“ Mimi nilipokea simu toka kwa Balozi nikiwa kanisani akinijulisha wananchi wameitisha kikao cha dharura na wananihitaji kwa haraka, ikanibidi nitoke kanisani nije kujua dhumuni la kikao, nilipofika nikawakuta wanachi wakiwa na Hasira sana kutokana na kiwanda cha (A to Z) kutiririsha maji machafu, yenye rangi ya sumu kwenye chanzo cha maji cha Mto Oloresho na wananchi walipanga kuandamana”
“Basi nikawaomba wananchi, tusichukua hatua ya haraka kabla yakuwa uthibitisho na uhakika wa jambo tulifanyalo, kwahiyo baada ya malumbano ya hoja ya muda mrfu tuliazimia, tukakague mfereji na madhara yaliyosababishwa na maji hayo, ndio unatuona tupo hapa mguu kwa mguu kukagua maji haya, eneo lililotengwa na Kiwanda kutitisha uchafu wote wa kiwanda”

Miundo mbinu ya barabara


“Tatizo hili ni la muda mrefu, hata mwaka jana wananchi waliandamana kwenda kwa Diwani, wakafika hadi kiwandani, kweli baada ya hayo maandamano kiwanda kikafunga maji haya kwa muda”
Aliendelea kueleza kuwa
“Tangu mvua zianze mwaka huu tumeona tena maji yenye rangi ya kutisha yakitiririka kluelekea kwenye makazi ya wananchi, mashama ya wananchi, mbaya zaidi ni kutiririkia kwenye Mto Oloresho, kwani Mto huu wananchi wanatumia maji hayo kwa kufulia, kuogea na Ng’ombe kunywa” alisema Mwenyekiti wa Mtaa wa Oloresho

Jamani tutapona kweli? Mifugo yetu, watoto wetu na sisi tu hatarini kwa hali hii.... ni maneno yaliyokuwa yakisemwa na wananchi hawa

0 Comments