Mzozo wa ubaguzi wa rangi unatokota nchini Ufaransa baada ya picha kupatikana za maafisa wa polisi wazungu wakiwa wamejipaka rangi nyeusi huku wakiiga mienendo ya nyani katika sherehe moja. Mkuu wa polisi wa Ufaransa ameanzisha uchunguzi juu ya suala hilo, baada ya picha hizo kupatikana katika ukurasa wa Facebook wa afisa mmoja wa polisi, imeripoti tovuti ya Channel 4. Maafisa hao wa polisi wanadhaniwa ni kutoka kikosi cha Kremlin-BicĂȘtre, kusini mwa Paris. Hii si mara ya kwanza kwa polisi wa Ufaransa kutuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii. Mwaka 2013 afisa mmoja wa kike wa polisi alitoa maoni ya kibaguzi hadharani.
|
0 Comments