Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva,
Kwa ufupi
- Akizungumza na viongozi wa dini jijini hapa jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, alisema tume hiyo imeanzisha mchakato wa kuboresha daftari hilo kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR), ili kuondoa hofu iliyopo.
Akizungumza na viongozi wa dini jijini hapa jana,
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, alisema tume hiyo
imeanzisha mchakato wa kuboresha daftari hilo kwa kutumia teknolojia ya
Biometric Voter Registration (BVR), ili kuondoa hofu iliyopo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa ni ukweli ulio
dhahiri kwamba teknolojia ya Optical Mark Recognation (OMR) iliyotumika
katika uchaguzi uliopita ilisababisha kasoro kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura hatua iliyosababisha wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake.
Alisema ameamua kuongea na viongozi hao wa dini
ili wakawaambie waumini wao kuwa zoezi hilo la usajili litakalochukua
siku 14 litaanza hivi karibuni.
“Vifaa kwa ajili ya zoezi hilo vimekwisha agizwa na Tume itavipokea Agosti, 2014 ili kuanza zoezi hilo.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa dini walihoji
uamuzi wa NEC kuwaomba kwenda kuwaambia waumini wao kwenye maeneo ya
ibada wakati wamekuwa wakizuiwa kuzungumzia masuala ya siasa katika
maeneo hayo.
Sheikh Mussa Kundecha kutoka Baraza Kuu la Jumuiya
na Taasisi ya Kiislamu, aliitaka NEC kueleza namna viongozi hao mpaka
uliopo baina ya dini na siasa: “Mmekuwa mkiwazuia viongozi wa dini na
siasa na mimi najua jambo hili halitaishia kwenye kujiandikisha tu,
litakwenda hadi kwenye uchaguzi, sasa tunatofautishaje na siasa?”
Akijibu swali hilo, Jaji Lubuva alisema: “ Tatizo
linakuwa pale unapowaambia waumini wakipigie kura chama fulani kwa
sababu kimeletwa na Mwenyezi Mungu.
0 Comments