Binti anayedaiwa kuteswa kwa kung’atwa na kuchomwa kwa pasi na mwajiri
wake, Yusta Lucas (kushoto) akilia pamoja na mama yake, Modesta Simon
katika Hospitali ya Mwananyamala jana, baada ya mama yake kuwasili
kutoka Tabora ili kumjulia hali.
Habari Kwa ufupi
Zilikuwa dakika 10 ngumu kwa mama huyo, Modesta
Simon kuamini hali aliyomkuta mwanaye aliyelazwa hospitali hapo kuuguza
majeraha kutokana na kufanyiwa ukatili na tajiri yake Amina Maige.
Kelele za vilio
jana zilisimamisha kwa muda shughuli katika Wodi ya Wanawake ya
Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam baada ya mama mzazi wa
msichana, Yusta Lucas (20) anayedaiwa kuteswa kwa kung’atwa na kuchomwa
kwa pasi mwili mzima kumwona mwanawe kwa mara ya kwanza.
Zilikuwa dakika 10 ngumu kwa mama huyo, Modesta
Simon kuamini hali aliyomkuta mwanaye aliyelazwa hospitali hapo kuuguza
majeraha kutokana na kufanyiwa ukatili na tajiri yake Amina Maige.
Mwanamke huyo anashikiliwa katika Kituo cha polisi
Oysterbay kwa tuhumu hizo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni
Thobias Edoyeka alisema leo atafikishwa mahakamani... “Bado sijafahamu
kama atapelekwa ama Kisutu au Kinondoni.”
Mara baada ya mama huyo kuingia katika wodi hiyo,
Yusta aliyekuwa ameketi kitandani aliruka na kumkimbilia mlangoni na
kilichofuata ni vilio.
Akizungumza huku akitokwa na machozi, Modesta
alisema: “Jamani Amina kweli amekufanya hivi, kila nikiuliza wananiambia
hujambo kumbe umeharibika hivi...”
Alisema habari za mateso na kulazwa kwa mwanaye alizipata kutoka kwa ndugu yake anayeishi Arusha...
“Alhamisi nilipata simu kutoa kwa ndugu yangu
Marieta Shitindi yeye anakaa Arusha, akaniambia ameona kwenye Mwananchi
na runinga kwamba Yusta amelazwa baada ya kupigwa na Amina ndipo
nikafunga safari kutoka Tabora kuja kuhakikisha.
Amina ni mtoto wa mjomba wangu kabisa na sikuwahi
kuambiwa chochote, niliamini wanaishi vizuri na sikudhani kama anaweza
kulifanya jambo hili.”
Modesta alisema awali alikuwa na mawasiliano na
mwanaye kupitia simu ya mama yake Amina ambaye wanaishi karibu, lakini
hivi karibuni alianza kupata wasiwasi baada ya kila alipohitaji kuongea
naye alipatiwa sababu hivyo akaomba Yusta kurudishwa na aliahidiwa
angepelekwa mwezi huu.
“Aliniahidi mwezi huu atamleta Yusta nyumbani
alisema anataka muda amnunulie na cherehani ili akija apate shughuli ya
kufanya...” alisema.
Ofisa Muuguzi katika wodi aliyolazwa Yusta, Erica
Massawe alisema hali ya binti huyo imeimarika na alisharuhusiwa kutoka
tangu Ijumaa iliyopita na kwamba wanasubiri maelekezo ya Polisi na
Ustawi wa Jamii kwani ndiyo wahusika wakuu.
|
0 Comments