Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, katika sikukuu ya wahisani ya umoja wa wanafunzi wa kikatoliki (TYCS), Dk. Slaa alisema kuwa, msingi mbovu wa elimu uliyopo ndiyo chanzo cha kuzalisha wasomi wengi lakini hawana sifa katika soko la Dunia.
“Mimi nashangaa kuona nchi hii inabadilisha mfumo wa zamani ambao ulikuwa ukimfanya mwanafunzi kujisomea kwa bidii na kupata wasomi walio na maarifa na uchungu na nchi yao, lakini hivi sasa mwanafunzi analetewa mtihani wa kuchagua majibu, huu ni uzembe kwa mamlaka husika,” alisema.
Aliongezea kuwa, wazazi nao wanapaswa kuwafuatatilia watoto wao kwa ukaribu katika masomo na maisha yao kwa ujumla, ili kuweza kutambua mapungufu ya mtoto na kuweza kuyatafutia ufumbuzi mapema.
Pia, aliwataka wazazi kuwapa fursa watoto endapo amegundua kuwa ana kipaji na kuweza kukiendeleza, kuliko kuona na kupuuzia jambo ambalo linaua ndoto zao.
Dk. Slaa, aliwataka vijana wote hususani wanafunzi, kutokujihusisha katika mambo mabaya yasiyompendeza Mwenyezi Mungu, yakiwemo ulevi, uzinzi, matumizi ya dawa za kulevya, rushwa na kuiga mambo ambayo hayana manufaa kwao, ili kuweza kutimiza ndoto walizonazo kwa manufaa ya kwao na taifa kwa ujumla.
Naye Katibu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam TYCS, Yohana Deogratias, alisema kuwa madhumuni ya umoja huo ni kuwasaidia wanafunzi kutambua haki na wajibu wao na kuweza kumjenga mwanafunzi kiroho.
Aliongezea kuwa, jimbo hilo lina kanda 16 na matawi 250, pia aliwataka wakuu wa shule na walezi kuweza kuwaruhusu wanafunzi kushiriki matukio mbalimbali ya chama hicho ili kuweza kuwajenga kiroho.
0 Comments