Hawa ni baadhi ya waandamanaji waliojipanga nje ya jengo la Mkuu Wa Mkoa wa Arusha kupaza sauti zao kwenda kwa Mh Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo.
Baada ya kuhowauliza kwa sharti la kutowataja majina, nini tatizo " Matapeli sana hawa, tulikuwa vibarua wa kusambaza umeme vijijini (REA), wametutapeli hawa" alisema kijana mmoja aliyeshika bango
Mwingine anasisitiza "hii kampuni ni yawatanzania bwana ila daah wametupiga, tumefuatilia mara kwa mara hawaeleweki" alisema kijana mwingine
Nadhani serikali ni sikivu wamepokea ujumbe huu na watusikilize kwasababu tumeteseka sana alisema muandamanaji mwingine. Mpaka naondoka eneo la tukio bado waandamanaji hawa walikuwa nje ya geti la kuingia ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
0 Comments