Zombe Aachiwa Huru, Mwenzake Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa
Mahakama ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, baada ya kumtia hatiani kwa kosa ka mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.
Wakati Bageni akihukumiwa kitanzi, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na maafisa wengine wawili wa Polisi, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari wameachiwa huru, baada ya mahakama kuwaona kuwa hawana hatia.
Bageni amehukumiwa adhabu hiyo leo baada ya mahakama ya Rufani kukubaliana na rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwaachia huru katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara hao.
Wafanyabiashara hao, Savings Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi wa Manzese, Juma Ndugu, waliuawa Januari 14,2006, kwa kupigwa risasi Mbezi Luis, Dar.
0 Comments