MCHEZO HUU UTUMIKE KWA KWA MANUFAA YA AFYA NA UCHUMI

Rais wa Shirikisho la karate nchini Tanzania na mkufunzi wa Karate mkoani Kilimanjaro Sensei Geofrey Kalonga


Rais wa Shirikisho la Karate nchini Tanzania ambaye pia ni mkufunzi mwandamizi wa Karate mkoani Kilimanjaro Geofrey Kalonga  aliyevaa vazi la Karate akiwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Ramadhani  Ng'anzi wakiwa kwenye tukio la kufunga mafunzo ya ya Gojukai Karate ya polisi Wilayani  Musoma hivi karibuni


Vijana wa Karate Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika picha na mkato unaojulikana kama Zenkutsudachi
Na.Vero Ignatus Kilimanjaro.

Katika kuadhimisho ya siku ya karate duniani wapenzi wa mchezo huo wametakiwa kuwa makini wasiutumie mchezo huo kama sehemu ya kufanyia uhalifu katika jamiii.

Hayo yamesemwa na Rais wa shirikisho la Karate nchini Tanzania ambaye pia ni mkufunzi wa karate mkoani Kilimanjaro, Sensei Geofrey Kalonga ,ambapo amesema kuwa mchezo huo wa karate ni kwaajili ya kujenga mwili kiafya na kujifunza mbinu mbalimbali za kuihami na wala siyo kutumia mchezo huo kuharibu lego lake. 
Aidha Kalonga amesema kuwa sambamba na kuadhimisha siku hii wanayofuraha kubwa kwani mchezo huo umeingizwa katika mashindano ya 0limpiki tofauti na miaka mingine ulikuwa hautambulikanai na watu wengi walidhania kuwa ni mchezo unaochezwa na wahuni tu.

“Hapo mwanzo mchezo huu ulikuwa unachuchuliwa kama ni wakujifunzia uhalifu au wanaoucheza ni vijana wa mitaani ambao hawana kazi ya kufanya jambo ambalo siyo sawa kabisa ni dhana potofu tu”alisema sensei.

Sensei kalonga amesema kuwa mchezo wa karate unachezwa na watu wa rika zote ,ambapo mchezo huo hauna kikomo unachezwa hadi uzeeni huku mchezaji afya yake ikizidi kuimarika zaidi.

Ameitaka jamii kuutambua mchezo huu kuwa ni mchezo kama ilivyo michezo mingine,kwani ni unakusaidia kujilinda mwenyewe,unaimarisha afya pamoja na mawasiliano kati ya ubongo na viungo mwili,ameitaka jamii haswa wanawake waondokane na dhana potofu kuwa ukicheza mchezo huo huzai kusema hivyo ni kukosa uelewa .



“Tunao wnawake wengi wancheza mchezo huu,ni wake za watu wanawatoto,na wanawake hawa wamefanya vizuri katika mshindano ndani na nje ya nchi yetu kuliko hata wanaume,hivyo wakina mama msirudi nyuma jiungeni mtapata faida kubw katika maisha yenu.

Aidha maadhimisho hayo ya karate hufanyika kila mwa Oktoba  22 ndiyo siku rasmi iliyoteuliwa kuwa siku ya karate duniani pote ambapo ilianzishwa karne ya 16  huko
Kisiwa cha Okinawa Nchini Japan.

0 Comments