ARDHI NI YAWATANZANIA, WAGENI MTUMIE KWA UWEKEZAJI TU- MH LUKUVI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Kwa ufupi

Akifungua kongamano la Chama cha Wapimaji wa Ardhi Tanzania (IST) jana, Lukuvi alisema hata watu walioukana uraia wa Tanzania wenye hati za kumiliki ardhi nao watanyang’anywa.

Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza vita dhidi wa raia wa kigeni wenye hati za kumiliki ardhi akisema sheria haiwaruhusu na akawaomba wananchi wamsaidie kuwafichua ili wanyang’anywe.

Akifungua kongamano la Chama cha Wapimaji wa Ardhi Tanzania (IST) jana, Lukuvi alisema hata watu walioukana uraia wa Tanzania wenye hati za kumiliki ardhi nao watanyang’anywa.

Lukuvi alisema wapo raia wa kigeni nchini ambao wana hati za kumiliki ardhi kinyume na sheria za nchi.

Alisema raia wa kigeni wanatakiwa kupewa ardhi kwa ajili ya matumizi ya uwekezaji tu na si kupewa hati za kumiliki ardhi wanayopewa.

0 Comments