CHUO KIKUU HURIA ( OUT) KUTUNUKU SHAHADA MFUNGWA AKIWA GEREZANI

Wahitimu hao ambao ni miongoni mwa zaidi ya 4,000 wa chuo hicho watakaotunukiwa katika ngazi tofauti ni Adamu Shabani (mlemavu wa kusikia) atakayetunukiwa Shahada ya Elimu Maalumu (BED Special Education); mfungwa kutoka Gereza la Butimba mkoani Mwanza, Machera Chacha, atakayetunukiwa Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi (DPTE) na mlemavu wa viungo, Dickie Mshani, atakayetunukiwa Shahada ya Lugha (BA English Language and Linguistics).

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo anawatunuku shahada za elimu ya juu wahitimu maalumu watatu kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT), akiwamo mfungwa na mwenye ulemavu wa kusikia.

Wahitimu hao ambao ni miongoni mwa zaidi ya 4,000 wa chuo hicho watakaotunukiwa katika ngazi tofauti ni Adamu Shabani (mlemavu wa kusikia) atakayetunukiwa Shahada ya Elimu Maalumu (BED Special Education); mfungwa kutoka Gereza la Butimba mkoani Mwanza, Machera Chacha, atakayetunukiwa Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi (DPTE) na mlemavu wa viungo, Dickie Mshani, atakayetunukiwa Shahada ya Lugha (BA English Language and Linguistics).

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda alisema jana kuwa wahitimu hao na wengine watatunukiwa wakati wa mahafali ya 31 yatakayofanyika eneo la chuo hicho Bungo wilayani Kibaha, Pwani.

Profesa Bisanda alisema licha ya Chacha kuendelea kutumikia adhabu, Gereza la Butimba limekuwa likimtumia kuwapa elimu wenzake. Alisema Rais Magufuli ndiye mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho (Taaluma), Profesa Deus Ngaruko alisema idadi ya wahitimu watakaotunukiwa ni 4,027.

Alisema wahitimu 20 wanatoka mataifa ya Kenya, Rwanda, Zambia, Namibia, Angola na Libya na miongoni mwao wawili watatunukiwa Shahada za Uzamivu, Shahada za Uzamili (watatu), Stashada ya Uzamivu (mmoja), Shahada ya Kwanza (13) na Stashahada (mmoja).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu na Usimamizi wa Teknolojia, Dk Edephonce Nfuka alisema kuwafundisha watu wenye ulemavu wa kuna changamoto kubwa lakini akasema kuwa wamekuwa wakifanikiwa kuwafundisha na kuhitimu kwa msaada wa Teknolojia ya Mawasiliano.

0 Comments