Mbunge wa Simanjiro Mhe. James Ole Millya Pamoja na naibu waziri wa Maji Mhe. Izack Kamwele wamezindua Mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Gunge kata ya Ruvuremit wilayani Simanjiro.
Vilevile Mbunge huyo wa Simanjiro pamoja na naibu Waziri wametembelea na kukagagua chanzo cha Maji kutoka mto Pangani na Mradi wa kupeleka Maji makao makuu ya wilaya ya Simanjiro ambao umbali wake ni kilomita 48 kutokea kwenye chanzo cha Maji.
Imetolewa na
Mozec Joseph
Afisa habari-Kanda ya kaskazini
0 Comments