KISMATY ADVERTY MEDIA YAZINDULIWA NA MEYA WA JIJI LA ARUSHA


Mh Kalist Lazaro amepongeza sana mkurugenzi wa Kismaty Marry Mollel, kwa ubunifu aliouanzisha na kuwa kampuni ya kwanza ya udalali wa habari, kimsingi kampuni hii itaturahisishia jinsi ya kupata wanahabari na vyombo vya habari alisema Mh Kalist Lazaro

Amempongeza sana Marry Mollel kuwa mwanamke wa kwanza kuanzisha  kampuni  nzuri sana itakayo tusaidia wote.

Mh Kalist Lazaro amewakumbusha kuwa makini na habari watakazo toa, ziwe za kweli, nzuri na kwa bora wakitambua sheria mpya ya Habari.

Mh Kalist Lazaro amemuunga mkono na kuunga mkono kazi zinazofanywa na Kismaty Advert Media kwa kuahidi kufanya kazi zake sasa kupitia kampuni yake, na kwa kuanzia ameahidi kuandaa kadi za kuwatakia Christmas na Mwaka Mpya mwema wananchi wa jiji la Arusha.

Kisha amezindua rasmi Kismaty Advert Media ili kampuni hii kuanza shughuli zao ili kukuza uchumi wa wananchini jiji wa Arusha.

0 Comments