Kwa ufupi
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Naif Company Limited (NCL) Khadija Naif Alyafei ambaye pia ni Balozi wa Utalii wa nchi za Uarabuni.
"Tulikuwa na maonesho ya Utalii hivi karibuni katika nchi za kiarabu ambapo tulikuwa tuonyesha bidhaa mbalimbali zinazopatikana Tanzania walivutiwa na mazao hayo na ikaonekana yanauhitaji mkubwa.”alisema.
Dar es Salaam. Mazao ya korosho, katani na chai yanayolimwa Tanzania yametajwa kuwa na soko nchi za Uarabuni.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Naif Company Limited (NCL) Khadija Naif Alyafei ambaye pia ni Balozi wa Utalii wa nchi za Uarabuni.
"Tulikuwa na maonesho ya Utalii hivi karibuni katika nchi za kiarabu ambapo tulikuwa tuonyesha bidhaa mbalimbali zinazopatikana Tanzania walivutiwa na mazao hayo na ikaonekana yanauhitaji mkubwa.”alisema.
Alisema mbali na mazao hayo pia nchi hizo zimevutiwa na vivutio vilivyopo nchini kama Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama na Kisiwa cha Zanzibar ambacho pia kilionesha kupendwa zaidi.
"Kutokana na maonyesho hayo kuwavuta waarabu wamependa kufanya biashara ya mazao hayo na kutembelea vivutio mbalimbali ni wakati sasa wa watanzania wenye makampuni kuwasiliana na mimi ili wapate fursa ya kuuza mazao na bidhaa zinazotokana na mazao hayo Uarabuni " alisema.
0 Comments