NILITAMANI MKE WANGU AENDE MAGEREZA- MH LEMA

Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini Neema Tarimo Amefikishwa Mahakamani ya hakimu mkazi Arusha mapema leo terehe 01-11-2016 Akikabiliwa na kile kinachodaiwa kuwa jina la usajili wa line ya simu iliyomtumia ujumbe wa kumtukana Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ilikuwa ni lake. Ujumbe uliodaiwakutumwa unasomeka "Karibu Arusha. Tutakudhibiti kama mashoga wanavyodhibitiwa  Uarabuni" 

Baada ya kufika mahakamani alisomewa shitaka la kumtukana Mkuu wa Mkoa, alikana shtaka na kuachiliwa huru kwa dhamana, shauri lilipangwa kusikilizwa siku nyingine

Mama Lema baada yakutoka mahakamani alisisitiza kuwa ujumbe aliouonyeshwa haukuwa wa matusi. "Nashangaa ata ujumbe wenyewe si wamatusi, kumuita mtu shoga mbona ni kawaida tu, shoga nineno wanawake tunatumia kuitana tukimaanisha rafiki, kwahiyo shoga sio tusi labda kama kunatafsiri tofauti aliyomaanisha" alisema Mama Lema 

Kwa upande wa Mbunge wa Arusha Mjini baada ya kumuwekea dhamana mkewe alisema "Kesi hii ni muendelezo wa jitihada ya serikali kuminya demokrasia na uhuru wa maoni binafsi ila tutashinda"

Aliendelea kusema "Nilitamani mke wangu aende akajue shida za wanawake wenzake magereza kwa kukaa siku 14 ndani ya magereza lakini madiwani wamenishauri sana nikaona tumdhamini tu" 

0 Comments