SHULE ZA NEEMEKA

Mbunge  wa  jimbo la Kilolo Venance  Mwamoto  wa tatu  kulia  akiongozana na kamati  yake ya mfuko  wa   jimbo  kukagua  miradi  ya kimaendeleo na  kuchangia  miradi  hiyo pichani ni  jengo la maabara ambalo limekwama  kuendelea  katika  shule ya  Sekodari Ipeta

Mbunge  Mwamoto  akitazama  shughuli  za ujenzi wa  vyoo katika  shule ya Msingi Iramba

Mbunge wa   kilolo Venance  Mwamoto  akikagua ujenzi wa choo  cha wanafunzi  shule ya Msingi Iramba  jana wakati wa  ziara  yake  ya ukaguzi  wa miradi  mbali mbali  jimboni  humo

Mwamoto  akikagua  ujenzi  wa kituo cha  Afya Ukumbi

Shimo  la choo  shule ya Sekondari Ipeta

Vyumba  vya madarasa  shule ya msingi Italula(P.T)

Vyoo  vya zamani  vya  wanafunzi  shule ya Msingi Kidabaga

Ujenzi  wa  vyoo  vya kisasa  shule ya Msingi Kidabaga  ukiendelea

Majengo  ya  shule ya Msingi  Kidabaga

Nyumba  ya  mwalimu Kidabaga  shule ya Msingi

Maabara  ya  shule ya sekondari Ipeta  ikiwa  imesimama  ujenzi  wake

Choo  cha mwalimu  mkuu  shule ya Msingi Mdeke  Kilolo

Na  MatukiodaimaBlog

MBUNGE wa  jimbo  la  Kilolo mkoani Iringa  Venance Mwamoto amechangia   zaidi ya Tsh milioni 20 kwa  ajili ya   kukamilisha miradi  mbaali  mbali  ya kimaendeleo  ikiwemo  ya  ujenzi  wa  vyoo vya  wanafunzi ,madarasa ,nyumba  za walimu na Zahanati  katika jimboni hilo  huku akiwataka viongozi  wa  serikali za  vijiji  na kata   kuhakikisha   wanakamilisha ujenzi  huo kwa wakati na  ubora .

Pamoja na kuwataka   viongozi hao  kusimamia ujenzi   huo amesema atachukua hatua  kali  kwa  kiongozi  yeyote  wa serikali ya  kijiji ama kata ambaye atatafuna  fedha   hizo   za ukamilishaji  wa miradi hiyo ya kimaendeleo jimboni   humo.

Mbunge huyo  aliyasema   hayo  jana  wakati  alipofanya  ziara  ukaguzi  wa miradi  9  inayoendelea  kwa  nguvu  za  wananchi  na Halmashauri  ya wilaya   ya  Kilolo na  kueleza  kuvutiwa na  miradi  hiyo japo kunahitajika  msukumo  wa haraka  katika umaliziaji  wa miradi   hiyo hasa ile  ya vyoo vya  wanafunzi ili kuwawezesha  wanafunzi hao  pindi shule  zinapofunguliwa kuwa na vyoo bora.

Alisema kutokana na  hali ya  hewa  kuwa mbaya  kwa  mvua  kuchelewa  kunyesha katika  maeneo  mbali mbali ya  wilaya ya  Kilolo tofauti na miaka mingine ameona ni  vema   kuwapunguzia makali ya michango wananchi wake  na badala  yake  sehemu ya  michango  ambayo  walipaswa kuchangia  ili  kukamilisha miradi  hiyo  kuibeba  yeye  kupitia  mfuko wa  jimbo kwa  kuchangia fedha  hizo.

Kwani alisema ni rahisi  kwa wananchi  kuchangia  nguvu  zao  kwa kushirikia  katika  ujenzi  huo  wa miradi  hiyo  kuliko kushiriki kutoa  fedha jambo  ambalo kwa wananchi hao  ni  sawa na  kuwatesa kutokana na  wengi   wao  waliuwa  wakiishi  kwa kutegemea  kilimo na hadi   sasa matumaini ya  kupata fedha  kwa njia ya  kilimo yametoweka baada ya  mvua  kushindwa  kunyesha  .

“Ninawaombeni sana  wananchi wangu  kwa sasa  ninyi  mshiriki  zaidi  katika maendeleo  kwa   kuchangia  nguvu  zenu  na mimi niwaunge  mkono kwa kuchangia  fedha  ili  kuifanya  miradi hii ikamilike  kwa  wakati”

Hata hivyo  alisema  kuna baadhi  ya maeneo wananchi  wanachangamoto  kubwa ya  barabara hasa  zile  zilizopo  chini ya  Halmashauri  kuwa barabara   hizo  zitafanyiwa matengenezo na  ile  ya Tanrod kutoka makao makuu ya wilaya ya  Kilolo  hadi Ndiwili mpakani  mwa jimbo  la Kalenga  inaanza kujengwa  kwa  kiwango  cha lami  mapema mwakani  na kuwa kuanzia January  ujenzi   huo  utaanza kwani  barabara   hiyo  ipo katika  ilani ya uchaguzi  ya CCM.

Mbunge Mwamoto  alisema  kuwa kwa suala la  ujenzi  wa Zahanati na vituo  vya afya  wananchi wamejitahidi  kwa maeneo mbali mbali aliyopita  kukagua ujenzi  umefikia  hatua  nzuri  na  kutolea mfano ujenzi  wa Zahanati ya Masege  ambao jengo  lake   bado  kuezekwa na  nyumba  ya mganga ipo  katika  hatua  ya  kuanza  kupandisha  kuta kuwa kukamilika kwa Zanahati   hiyo  kutawawezesha  wananchi  hao  ambao  walikuwa wakilazimika  kufuata matibabu Kibengu na  Usokami  wilaya ya  Mufindi wataweza  kutibiwa katika Zanahati   hiyo.

Alisema katika ziara  yake  hiyo aliyoambatana na  wajumbe  wa mfuko  wa jimbo kupitia  fedha  za  mfuko wa   jimbo   Kijiji cha Mdeke ambako kuna ujenzi  wa vyoo  vya  wanafunzi  amechangia  Tsh milioni 1 na kwenye ujenzi wa  nyumba ya  mwalimu  amechangia  Tsh milioni 2 ,  sekondari ya Ipeta kwa  ajili ya  ujenzi  wa vyoo  vya  wanafunzi  amechangia Tsh  milioni 2, shule ya Msingi Kidabaga amechangia Tsh  milioni  3 kwa ajili ya vyoo na nyumba  ya  mwalimu ,Wangama  amechangia  Tsh milioni 1 kwa  ajili ya ukarabati  wa madarasa ,Kitongoji  cha Ifiga amechangia Tsh milioni 1 kwa  ajili ya  kuanzisha mkondo  B wakati ujenzi  wa Zahanati na nyumba ya  Mganga  Masege am

0 Comments