JE UZOEFU UNATIJA KATIKA MAFANIKIO YAKO?

Na Elisha Edson, Iringa

Miaka mitatu ya kufanya kazi katika utalaamu fulani ni kigezo cha kutosha kumpa mtu sifa za kuitwa ana uzoefu kwa hiyo kazi ambayo amekuwa akifanya? Kwa kweli, kujihusisha kwa kuwa na mwendelezo wa kufanya jambo hilohilo kwa miezi 36 ni kitu cha kutosha kumweka huyo mtu kwenye kina na upana wa uhalisia ulio kwenye utalaamu wowote. Hii ndiyo maana, vyuo vingi hutoa stashahada au shahada za chuo kikuu kwa program za ndani ya miaka 3 na fursa nyingi za kazi katika nafasi za uandamizi au nafasi za juu zinahitaji kigezo cha uzoefu wa walau miaka 3.

Sasa basi, tukiongelea miaka 14 au zaidi kumwita mtu nguli (veterani) wa eneo lake la utaalamu; Watu ambao wamefanya kazi kwa muda mrefu kabisa huitwa wataalmu wabobezi (experts). Mara nyingi huwa wanaheshimika na baadhi ya wanajamii kutamani uwezo au hatua waliyofikia hasa wale walio katika eneo moja la kiutaalamu (specialization). Watu hawa wanakuwa wamefanya majaribio ya karibu kila kitu katika maeneo yao ya kitaalam, na hivyo inakuwa vigumu kuwa na swali kwenye kazi zao. Mara nyngi hufuatwa na asasi za kitaifa au kimataifa kwa ajili ya kutoa ushauri wa kitaalamu (consultation) kwa lengo la kitatua matatizo magumu katika eneo lao la kitaalamu. Watu hawa hufurahia kiwango cha juu cha hadhi ya utaalamu waliyonayo hali kadhalika jamii nayo hufurahia hadhi yao. Kutokana mafanikio na kiwango cha hadhi yao katika jamii walichofikia watu hawa kama hawatakuwa wanyeyekevu wa kutosha mara nyingi huangukia katika undanganyifu wa kifikra kwa kujiona wanajua kila kitu kwa kiwango cha kutotaka tena kujifunza kitu chochote kipya.

Wanakuwa wakosoaji (critical) na wagumu kuamini (cynical) njia mpya za kufanya vitu na mara nyingi wenye ushawishi (influence) na si wenye mafanikio (affluent)!
Hii ilitokea kwa kijana mdogo alieitwa Yakobo. Alifanya kazi kwa mjomba wake akiwa kama Afisa Mkuu wa Kutunza Mifugo (Chief Animal Husbandry Officer – CAHO) kwa miaka 14 kwa mshahara wa wake wawili. Jamaa huyu alikuwa na shauku na mwenye kuipenda kazi yake na kufanya vizuri sana kwa kuwa alikuwa kwenye taaluma hiyo tangu akiwa na mvulana. Hivyo basi, miaka 14 ilikuwa kama siku 14 tu, kwa kupiga kazi kwa ajili ya mke wa ndoto zake alieitwa Rehel.
Japokuwa alimtumikia mjomba wake kwa zaidi ya miaka 14 na kupata uzoefu wa kutosha kama mtaalamu wa mifugo, ila maisha yake kiuchumi hayakuwa na kitu chochote cha kujivunia nyumbani kwake. Kile alichokuwa nacho ni wake wawili, wanawake wengine wawili aliozaa nao nje ya ndoa (ambao kwa hali ya leo ni wanawake wasaidizi wa kazi za ndani ) na watoto 11 wa kiume (kumbukumbu pia zinamtaja binti mmoja tu wa kike aliekuwa anaitwa Dina). Yakobo hakumiliki mali yake mwenyewe inayohamishika au isiyohamishika. Kama wasifu wange ungeandikwa basi, ingesomeka, “Niliongeza mifugo ya mjomba wangu kutoka katika uchache kwende kwenye wingi”. Baada ya kuishi katika umasikini na kutokuwa na fedha, licha ya uzoefu wake kwa kazi aliyokuwa akiifanya, siku moja alimfuata muajiri wake, mara hii si kwa kuomba ongezeko la ujira (au mshahara) au kwa mafao mengine kama alivyokuwa akifanya huko nyuma.

Yakobo alimwambia muajiri wake,
“Usinipe kitu; ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda. Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu. Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.”

Ikawa mwanzo wa kujua kuwa uzoefu wake haujamsaidia kama ambavyo alifikiri. Alihitaji kufanya kitu kingine cha ziada nacho ni MABADILIKO. Alibadilika kutoka kuwa mtu wa akili ya kutegemea mshahara na kuwa na akili ya kijasiliamali. Na pia, akaja na mkakati uliomfanya mmoja wa watu wenye utajiri mkubwa katika wakati wake. Na alikuja kuwa tajiri kuliko Laban ambae ni muajiri wake ndani ya muda si mrefu kitu kilichopelekea wawili hawa kutofautiana na kila mmoja kuchukua “hamsini” zake kwasababu ya wivu uliozaa chuki kutoka kwa muajiri wake ambae pia alikua mjomba wake.

Kilifanya tofauti katika maisha ya kiuchumi kwa Yakobo haikuwa uzoefu, bali kubadili kwa MTAZAMO na MKAKATI.
“Kwa hiyo mtu huyo (yaani Yakobo) akafanikiwa mno, akawa na wanyama wengi, na wafanyakazi wa kike, na wafanyakazi wa kiume, na ngamia, na punda.”

Badiliko la kimtazamo na kimkakati linawezekana kwako wewe unaesoma makala hii na ndicho kitu unachohitaji ili uwe mtu yule ambae umekuwa ukitaka kuwa. Ili uwe na biashara ambayo nyakati zote umekuwa ukifikiri unahitaji, ili uwe na aina ya ushawishi (influence) na mafanikio (affluence) ambao umekuwa mara zote ukitamani uwe nao, na muhimu zaidi, kiwango bora cha maisha ambacho mara zote umekuwa ukiota uwe nayo.

Badili mtazamo na mkakati wako na uone kwa namna abavyo wazo lako, biashara, mahusiano na kazi yako itabadiika. Acha kujisifia uzoefu wako badala yake fanya tathmini ya namna gani imekusaiia kufikia malengo yako.
Ndiyo, uzoefu ni muhimu, lakini, mtazamo na mkakati sahihi ndiyo wenye maana zaidi kusaidia kutimiza malengo yako ambayo yatakufikisha katika ndoto zako maishani.
Kumbuka sehemu ya hadithi imetoka katika biblia, Mwanzo 29-32

Makala hii imeandikwa kwenye ukurasa wake wa facebook kwa lugha ya kingereza na kutafsiriwa na Fredrick Matuja kwa ruhusa ya "author" ambae ni Elisha Edson. 

0 Comments