VIONGOZI WATAKAOSHIRIKI KUZUIA WANAFUNZI KWENDA SHULE KUKAMATWA- MONDULI


Halmashauri ya  wilaya ya Monduli imeanza kutekeleza mpango wa kuwakamata wenyeviti  wa vitongoji wanaoshirikiana na wazazi kutoka jamii ya kifugaji kuwatorosha watoto wenye umri wa kuandikishwa darasa la kwanza ili wakachunge mifugo hali inayotajwa kudumaza juhudi za serikali ya wamu ya tano ya kutoa elimu bure kwa watoto wa kitanzania.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli Steveen Ulaya ametoa kauli hiyo kwenye uzinduzi wa mabweni mawili ya wanafunzi wa shule ya msingi Mbashi kata ya Selela yaliyojengwa na wadau wa elimu ili kuwasaidia wanafunzi wa jamii ya kifugaji huku akitoa wiki moja kwa watendaji kupeleka takwimu ya wanafunzi waliyoandikishwa kwa mwaka huu.

Diwani wa kata ya Selela Cathibert Meena amesema mpango huo unatekelezwa kwa mujibu wa sheria na utawagusa mwenyeviti wa vitongoji na wazazi kwakuwa tabia hiyo imekuwa sugu na mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema mabweni hayo yatasaida kupunguza utoro kwa wanafunzi.

Wadau wa elimu kutoka shirika la kiholanzi la Tanzania Suport Foundation na mtandao wa wafugaji Tanzania TPCF wamesema lengo la kujenga mabweni hayo ni kupunguza changamoto za elimu kwa watoto wa kifugaji wanatembea zaidi ya kilometa ishirini kutoka kwenye makazi hadi shuleni hapo.

0 Comments