Mbali ya majengo yanayoendelea kujengwa na kuongeza mvuto na muonekano mpya wa UDSM bila kuathiri mandhari ya chuo kinachozungukwa na miti ya asili katika eneo hilo maarufu la Mlimani, pia mabadiliko mengine ni ongezeko la fani mbalimbali katika kila nyanja.
Dar es Salaam. Mabadiliko makubwa yanaendelea kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kujenga majengo mengi ikiwamo maktaba kubwa ya kisasa itakayoweza kuchukua wanafunzi 2,100 kwa wakati mmoja.
Mbali ya majengo yanayoendelea kujengwa na kuongeza mvuto na muonekano mpya wa UDSM bila kuathiri mandhari ya chuo kinachozungukwa na miti ya asili katika eneo hilo maarufu la Mlimani, pia mabadiliko mengine ni ongezeko la fani mbalimbali katika kila nyanja.
Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu juzi, Naibu Makamu Mkuu wa UDSM-Utawala, Profesa David Mfinanga anasema yote hayo yanaendelea kwa kuwa wanataka kuwa ‘comprehensive univeristy’ yaani chuo kinachojitosheleza kwa kufundisha fani mbalimbali katika kila nyanja.
“Tunataka kuwa hivyo ili tuweze kushirikiana fani moja na nyingine kwa karibu kwa kuwa vyuo vya aina hiyo vinahitajika sana ulimwenguni,”anasema Profesa Mfinanga na kuongeza kuwa na chuo cha aina hiyo kunasaidia hata mtu aliyeko nje ya nchi ambaye anataka kuwekeza nchini ajue wapi atapata nguvu kazi.
Katika kubadilika huko hivi sasa UDSM ina chuo cha afya na kilimo ambavyo vinaongeza wigo wa fani mbalimbali katika chuo hicho. “Nia ya kufanya hivi ni ili pia tuweze kufanya tafiti ambazo zitakuwa zinaleta matokeo tofauti,” anasema.
 
0 Comments