ELIMU YA UONGOZI NA BIASHARA YATOLEWA


Katibu Mkuu wa Kingdom Leadership Network Tanzania Charles Sokile akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maandalizi ya mkutano wa pili wa kiuchumi na kuwataka viongozi mbalimbali kujitokeza, Kulia ni Mwanzilishi wa KLNT Issac Mpwata na Kushoto ni Afisa masoko  Carol Maajabu

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Shirika lisilo la kiserikali la Kingdom Leadership network Tanzania (KLNT) limeandaa mkutano wa pili wa Tanzania National Prayer Breakfast na mkutano wa Kiuchumi ujulikanao kama 2017 Kingdom Economic Summit.

Mkutano huo utakaofanyika kuanzia machi 6-8 utajumuisha shirika la huduma la kimataifa ya Bill Winston kutoka nchini Marekani na unatarajiwa kuhudhuriwa na Makamu wa Raisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Samia 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, katibu mkuu wa KLNT Charles Sokile amesema kuwa mkutano huo wa uchumi unatoa nafasi ya kipekee kwa watu binafsi, wafanyabiashara, mashirika ya kibiashara na viongozi wa makanisa kuweza kujipatia ujuzi na uzoefu kutoka kwa wasemaji mkuu wa mkutano mkuu.

"Tunajivunia kuweza kuleta tena mkutano huu kwa mwaka wa pili sasa na kuweza kuleta wageni rasmi ili kuja kuhamasisha watanzania na kuleta mabadiliko chanya kimaadili katika uongozi na biashara kwa mtu mmoja mmoja na hatimaye taifa kwa ujumla," amesema Sokile.

Mwanzilishi wa KLNT Isaac Mpwata amesema kuwa kila mara wanajikita katika kuhakikisha wanatoa fursa za mafunzo ya kiongozi na biashara yanayojikita kwenye suala zima la maadili kama msingi wa mafanikio.

Mpwata amesema kwa kupitia mkutano huu wanategemea kuendelea kujenga uwezo wa viongozi wetu na wafanyabiashara kwa ajili ya kubadili taifa letu kwa kutumia kanuni za uongozi wa kimaadili ili kuleta mabadiliko chanya katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

0 Comments